1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin alisifu jeshi lake, asema hakuna wa kuwarudisha nyuma

31 Desemba 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi amelisifu jeshi la nchi hiyo katika salamu zake kwenye mkesha wa mwaka mpya huku akitoa wito wa umoja.

Rais Vladimir Putin amesema mwaka wa 2024 utakuwa ni mwaka wa familia
Rais Vladimir Putin alipohudhuria mkutano wa Bodi ya Wizara ya Ulinzi katika Kituo cha Usalama wa Taifa mjini Moscow, 19.12.2023 Picha: Sputnik/Mikhail Klimentyev/Kremlin via REUTERS

Rais Vladimir Putin ametoa matamshi hayo katika hotuba ambayo haikuwa na maneno makali na ambayo haikuutaja mzozo wa Ukraine.

Tofauti na mwaka uliopita, Putin aliyehutubia kutoka Ikulu ya Kremlin ameuelezea mwaka 2024 kuwa ni mwaka wa familia.

Putin amesema kwenye hotuba hiyo iliyorushwa kwenye televisheni kwamba mara kadhaa wamethibitisha kuwa wanaweza kutatua matatizo makubwa wao wenyewe na hawatakatishwa tamaa kamwe kwa kuwa hakuna anayeweza kuwatenganisha, huku akiwamwagia sifa wanajeshi walio vitani.

Hotuba hiyo ya mkesha wa mwaka mpya ni mwendelezo wa utamaduni ulioanzishwa na kiongozi wa kisovieti Leonid Brezhnev na hutizamwa na mamilioni ya wakazi wa Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW