1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Putin ampongeza Xi kwa kuongezewa muhula wa tatu madarakani

10 Machi 2023

Rais wa Urusi, Vladmir Putin amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa kuongezewa muhula mwingine wa tatu madarakani wa miaka mitano

China Peking | Wladimir Putin und Xi Jinping Februar 2022
Picha: Alexei Druzhinin/AP/picture alliance

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Urusi, Kremlin, imeeleza kuwa Putin amemwambia Xi kwamba ana uhakika viongozi hao wawili wanaweza kuimarisha ushirikiano wao  katika masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

Kwa mujibu wa Putin, anaamini kwamba watafanya kazi pamoja na watahakikisha kwamba wanatanua ushirikiano wa kimkakati kati ya Urusi na China katika nyanja mbalimbali.

Bunge la Umma wa China, NPC leo limemchagua Xi kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu, na kumfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi China tangu utawala wa Mao Zedong. Bunge hilo pia limemchagua Zhao Leji kuwa spika wake na Han Zheng kuwa makamu mpya wa rais.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW