Putin amuonya Bush dhidi ya kuteka mitambo yake Poland na katika jamhuri ya Tcheki
12 Oktoba 2007Moscow:
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice na waziri mwenzake wa ulinzi Robert Gates wamewasili Moscow kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa kisiasa wa Urusi.Mawaziri hao wawili wa Marekani wamepangiwa kwanza kuzungumza na rais Vladimir Putin.Uhusiano kati ya pande hizi mbili umeingia dowa kutokana na mipango ya Marekani ya kutega mitambo ya kinga ya makombora nchini Poland na katika jamhuri ya Tcheki pamoja na suala la vikwazo dhidi ya Iran.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice amesema kabla ya kuwasili mjini Moscow,Marekani itaendelea na mipango yake ya kutega kinga ya makombora,lakini iko tayari kusikiliza mapendekezo ya Urusi.Rais Vladimir Putin alipendekeza mwezi July uliopita,Marekani itumie mtambo wa radar uliowekwa katika kituo cha Urusi nchini Azerbaidjan.Kiongozi huyo wa Urusi ameitahadharisha Marekani dhidi ya kutekeleza kwa nguvu mpango wake.