1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin aonya juu ya Kyiv kutumia makombora ya masafa marefu

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Rais Vladimir Putin amesema wizara ya ulinzi ya Urusi inafanyia kazi njia tofauti za kujibu endapo Marekani na washirika wake wa Jumuiya ya NATO, wataisaidia Ukraine kufanya mashambulizi ya masafa marefu ndani ya Moscow.

Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir PutinPicha: Sergey Bobylev/Sputnik/REUTERS

Rais Vladimir Putin amesema leo kwamba wizara ya ulinzi ya Urusi inafanyia kazi njia tofauti za kujibu endapo Marekani na washirika wake wa Jumuiya ya NATO, wataisaidia Ukraine kufanya mashambulizi ya masafa marefu ndani ya Moscow kwa kutumia silaha za Magharibi. Soma: Putin asema Marekani itaamua yenyewe uhusiano baina yao

Vita vya miaka miwili na nusu vya Ukraine, vimesababisha msuguano mkubwa baina ya Urusi na nchi za Magharibi tangu vita baridi.

Maafisa wa Urusi wanasema vita hivyo sasa vinaingia katika awamu yake ya hatari zaidi. Kwa wiki kadhaa Urusi imekuwa ikitoa ishara kwa Marekani na washirika wake kwamba, ikiwa wataipatia idhini Ukraine ya kutumia makombora yake ya masafa marefu kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi, huenda Moscow ikifikiria kufanya mashambulizi makubwa ya kulipa kisasi.

Putin aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hatua kama hiyo itamaanisha ungiliaji kati wa moja kwa moja wa NATO, Marekani na nchi za Ulaya katika vita vya Ukraine.