1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aonya nchi za magharibi dhidi ya kuipa Ukraine silaha

3 Februari 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameapa kuwa atajibu vikali dhidi ya taifa lolote linalotishia usalama wa Urusi.

Russland-Militär | Präsident Wladimir Putin
Picha: Mikhail Klimentyev/Sputnik/Kremlin/AP Photo/picture alliance

Rais Putin ametoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake kwenye kumbukumbu ya miaka 80 tangu jeshi la uliokuwa Muungano wa Kisovieti kupata ushindi dhidi ya vikosi vya Ujerumani kwenye mapigano ya kuwania mji Stalingrad mashariki mwa Urusi.

Ametumia hotuba hiyo pia kuikosoa Ujerumani kwa uamuzi wake wa kuipatia Ukraine vifaru vya kisasa vya Leopard 2 akiifananisha hatua hiyo kuwa sawa na kitisho kipya kutoka kwa Ujerumani kama ilivyokuwa wakati vita vikuu vya pili vya dunia.

Hotuba hiyo ya Putin inafuatia tahadhari iliyotolewa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliyesema kwamba ikulu ya Kremlin inaimarisha nguvu ya vikosi vyake ili kuanzisha wimbi jipya la mashambulizi nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW