1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Naamini Urusi itashinda vita vyake dhidi ya Ukraine

31 Desemba 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameelezea imani ya kushinda vita ya Ukraine katika hotuba yake ya mwaka mpya, baada ya miaka minne ya vita vyake na Kiev.

Russland Moskau 2025 | Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Vladimir Smirnov/TASS/ZUMA/picture alliance

Putin amewapongeza wapiganaji na makamanda akisema anawaamini na anaamini taifa hilo litashinda vita hivyo.

Wanajeshi wake ambao Ukraine imewashutumu kutekeleza uhalifu wa kivita wamesifiwa na Putin aliyewaita mashujaa.

Putin ameyasema hayo wakati kukiwa na wasiwasi wa kutanuka kwa mgogoro huo baada ya Urusi kudai Ukraine imeshambulia makaazi ya Putin kwa droni hatua iliyoiita ya kigaidi na inayochochea kudhoofisha juhudi zinazoendelea za amani.

Licha ya hayo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alisema atakutana na washirika wake Januari 6 nchini Ufaransa katika juhudi za kuendeleza juhudi za kusaka amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW