1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin asema Prigozhin alikataa kuwachia kamandi ya Wagner

14 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema mkuu wa kampuni ya mamluki ya Wagner Yevgeny Prigozhin alikataa kuwaruhusu wapiganaji wake kuhudumu chini ya amri ya mtu mwengine, jambo ambalo lingetatua hatima ya kundi hilo.

Kombo Prigohzin Putin
Picha: picture alliance

Wiki tatu baada ya Prigozhin kuanzisha uasi wa muda mfupi dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Urusi, mustakabali na mahali waliko wanajeshi wa Wagner bado havijulikani.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti moja, Putin alisema alikuwa amewapa chaguo mwafaka wapiganaji wa Wagner.

Aliwataka wajikusanye sehemu moja na kuendelea kuhudumu chini ya amri ya kamanda aliyepewa jina Sedoy.

Kwa mujibu wa Putin, wengi walikubali lakini Prigozhin akakataa ofa hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW