1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Putin asema Ukraine itapokea jibu stahiki uvamizi Kursk

13 Agosti 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameliagiza jeshi lake jana kuwatimua wanajeshi wa Ukraine walioingia ardhi ya Urusi, huku maafisa wakisema zaidi ya watu 120,000 wameondolewa kwenye eneo la mapigano.

Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir PutinPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Kyiv ilifanya shambulio la kustukiza ndani ya mkoa wa magharibi mwa Urusi wa Kursk Jumanne jioni, na kuteka maeneo zaidi ya 25, katika shambulio kubwa zaidi kwenye ardhi ya Urusi tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Mkuu wa majeshi ya Ukraine Oleksander Syrsky alimuambia Rais Volodymyr Zelenskiy katika vidio iliyochapishwa Jumatatu, kuwa vikosi vyake vinadhibiti karibu kilomita za mraba 1,000 za ardhi ya Urusi na vinaendeleza mashambulizi.

Miaka 25 ya Putin madarakani na ushawishi wa Urusi Afrika

02:17

This browser does not support the video element.

Putinameuambia mkutano wa maafisa wa serikali kwamba moja ya malengo ya wazi ya adui ni kuchochea mfarakano na kuharibu umoja na mshikamano wa jamii ya Urusi, na kuonya kuwa Ukraine itapokea jibu linalostahili.