1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin yuko tayari kuujadili mpango wa China kuhusu Ukraine

21 Machi 2023

Rais Vladmir Putin amemwambia mwenzake wa China Xi Jinping kuwa Urusi iko tayari kuyajadili mapendekezo ya China ya kumaliza mapigano nchini Ukraine.

Russland Präsident Xi und Putin
Picha: Sergei Karpukhin/Sputnik/REUTERS

Putin aliyasema hayo jana mwanzoni mwa mazungumzo yao mjini Kremlin. Mkutano huo wa kilele unafanyika wakati China ikitafuta kujiweka kama nchi isiyoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine, lakini Washington imeonya kuwa ulimwengu haupaswi kudanganywa na hatua za Beijing.

Marekani inaituhumu Beijing kwa kuiuzia Moscow silaha, madai ambayo China inayakanusha vikali.Ziara ya Xi ni yake ya kwanza mjini Moscow  tangu kuanza kwa uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine mwaka jana. Xi alisifu mahusiano ya karibu na Urusi naye kiongozi huyo wa Urusi akasema nchi hizo mbili zina malengo na majukumu mengi ya pamoja.

Putin na Xi watakutana tena leo kwa mazungumzo rasmi. Lakini Kyiv hapo jana imerudia wito wake kwa Urusi kuviondoa vikosi vyake Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW