1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin atangaza sheria za kijeshi mikoa minne Ukraine

Hawa Bihoga19 Oktoba 2022

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza sheria za kijeshi katika mikoa 4 ya Ukraine ambayo ilinyakuwa hivi karibuni katika utaratibu ambao haukukubaliwa kimataifa na ametoa mamlaka ya ziada kwa wakuu wa mikoa yote.

Russland | Sitzung Sicherheitsrat | Wladimir Putin
Picha: Sergei Ilyin/SPUTNIK/AFP/Getty Images

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni wiki chache baada ya kuishambulia miji ya Ukraine ikiwemo ile ya kimkakati na kusababisha vifo vya watu kadhaa huku miundombinu ya huduma za kijamii ikiharibiwa.

Rais Putin katika tangazo lake hakutaja mara moja hatua ambazo zingechukuliwa chini ya sheria ya kijeshi lakini amesema agizo lake liaanza kutekelezwa siku ya Alkhamis.

 Amri ya Rais Putin inavipa vyombo vya sheria siku tatu kuwasilisha mapendekezo maalum na kuamuru kuundwa kwa eneo la vikosi vya ulinzi katika mikoa minne  liyounyakuliwa na na nchi yake.

Katika hotuba yake ya televisheni Putin  alitangaza mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Donetsk, Luhansk, pamoja na mikoa ya  Kherson na Zaporizhzhia,.

Putin ameongeza kwamba kabla na mikoa hiyo haijajiunga na Urusi sheria ya kijeshi ilikuwa inafanya kazi na sasa kilichobaki ni kurasimisha mikoa hiyo kuingia kwenye mfumo wa sheria za Urusi.

Soma zaidi:Urusi kuhamisha watu 10,000 kwa siku kutoka Kherson

ameelekeza maafisa wake kutoa kipaumbele katika kutekelezwa kwa hatua hiyo iliofikiwa  ili kuhakikisha usalama unaimarishwa kwa nyanja zote.

"kutoa kipaumbele katika hatua hii na  kuongeza utulivu wa kiuchumi, kuanzisha na kutanua uzalishaji wa bidhaa muhimu kwa oparesheni maalum ya kijeshi."

Rasimu ya sheria hiyo inaonesha kuwa inaweza kuhusisha vikwazo vya kusafiri na mikusanyiko ya umma pamoja na udhibiti mkali na mamlaka makubwa kwa vyombo vya sheria.

Ukraine yapuuza tangazo la Putin

Kufuatia hatua hiyo ya Urusi Mshauri wa Rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak kupitia mtandao wa twita amepuuzilia mbali tangazo hilo la Rais Putin.

Pichani ni Rais wa Urusi Vladimir Putin na Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Russia/Ukraine Press Offices/AP/picture alliance

Ameandika kwamba huo ni uhalalishaji wa uwongo wa uporaji wa mali za Ukraine na kuongeza kwamba hatua hiyo haibatilishi chochote kwa Ukraine.

mshauri huyo wa rais Zelensky amendelea kusema kwamba wataendelea na juhudi zao za ukombozi na kurejesha maeneo yaliotwaliwa na Urusi.

EU: Kunaushahidi Iran kuipa drones Urusi

Katika hatua nyinge serikali za Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuweka vikwazo kwa muda kwa watu wanane na taasisi za Iran baada ya ndege zisiszokuwa na ruban zilizotengenezwa Iran kutumiwa na vikosi vya Urusi kushambuliaUkraine.

Ukraine iliripoti mkururo wa mashambulizi ya Urusi kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani za shahed-136 zilizotengenezwa na Iran katika wiki za hivi karibuni hatua ambayo Iran imekanusha vikali wakati ikulu ya Kremlin haijatoa tamko lolote juu ya shutuma hizo.

Soma zaidi:Urusi yazidi kuishambulia Ukraine kwa Makombora ya angani

Msemaji wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya amesema kuna makubaliano ya kisiasa ya pamoja yalioafikiwa na mawaziri wa mambo ya nje wanaokutana mjini Luxembourg, kwamba Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kutokana na ushahidi wa kutosha iliopata juu ya shutuma hizo dhidi ya Iran.

Urusi yaendelea kushambulia miji ya Ukraine kwa makombora

01:44

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW