1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin ateuwa gavana mpya wa Kursk

6 Desemba 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amemteuwa gavana mpya wa mkoa wa Kursk, ambao sehemu yake ipo ndani ya Ukraine.

Vladimir Putin, Urusi
Rais Vladimir Putin wa Urusi.Picha: Ramil Sitdikov/AP Photo/picture alliance

Alexander Khinshtein, mwandishi wa habari aliyeingia bungeni mwaka 2003, anachukuwa nafasi ya Alexei Smirnov, ambaye alishikilia nafasi hiyo mwezi Mei akiungwa mkono na Ikulu ya Kremlin.

Mnamo majira ya kiangazi ya mwaka huu, jeshi la Ukraine lilifanya uvamizi wa kushitukiza dhidi ya mkoa wa Kursk, na kupelekea hasara kubwa kwa Urusi.

Soma zaidi: Rais Zelensky aitaka Marekani iushawishi Umoja wa Ulaya ukubali kuikaribisha Ukraine NATO

Uteuzi wa Khinstein unachukuliwa na wengi kama ishara ya mageuzi makubwa kwenye mfumo wa ulinzi wa Urusi, hasa kutokana na ukweli kwamba kwa miaka miwili alikuwa mshauri kwa mkuu Kikosi Maalum cha Ulinzi wa Rais.

Vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu kuwaondosha wanajeshi wa Ukraine kwenye mkoa wa Kursk kwa miezi kadhaa sasa.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaripotiwa kutumwa kwenye mkoa huo kuisaidia Urusi, kwa mujibu wa duru za kijasusi za Magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW