SiasaMongolia
Putin atoa mwaliko kwa Mongolia kuhudhuria mkutano wa BRICS
3 Septemba 2024Matangazo
Rais Vladimir Putin anayefanya ziara nchini Mongolia amesema anadhamiria hasa kuzungumzia juu ya ushirikiano wa kiuchumi na Mongolia.
Ziara ya Putin nchini Mongolia inazingatiwa kuwa ya utata kwa sababu Mongolia inaitambua mahakama ya kimataifa iliyotoa waranti wa kuwezesha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Urusi.
Soma pia: Putin asema uvamizi wa Ukraine Kursk haujawa na athari
Hata hivyo hakuna dalili kwamba nchi hiyo mwenyeji itatekeleza wito wa kumkamata rais huyo wa Urusi kwa madai ya uhalifu wa kivita kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Mongolia inayopakana na Urusi inamtegemea sana jirani yake huyo kwa mafuta na umeme.