1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Putin avunja ukimya kuhusu kifo cha Prigozhin

25 Agosti 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amevunja ukimya kuhusu ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua kiongozi wa kundi binafsi la kijeshi la nchi hiyo, Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sergei Bobylev/TASS/imago images

Putin amethibitisha lakini sio moja kwa moja kifo cha kiongozi huyo siku moja baada ya ndege aliyoaminika kusafiria kuanguka kwenye mji wa Tver nchini Urusi.

Katika ujumbe aliyoutoa kwa njia ya vidio kwa Prigozhin aliyekuwa mwandani wake wa karibu ambaye wanajeshi wake walikuwa na jukumu muhimu kupambana na vikosi vya Ukraine, Putin alimuelezea kama kiongozi aliyekuwa na talanta, aliyefanya makosa makubwa katika maisha yake lakini pia aliyefanikiwa kuleta matokeo yaliyohitajika.

Zelensky: Hatuhusiki na ajali ya ndege inayodaiwa kumuua Prigozhin

Wachambuzi wanasema ni vigumu kubaini iwapo kiongoui huyo wa wagner ameuwawa au la. Taasisi ya Serikali ya Urusi inayohusika na masuala ya usafiri wa anga ilisema Prigozhin, pamoja na kamanda wa juu wa kundi la wagner Dmitri Utkin, ni miongoni mwa watu 10 waliokuwepo katika ndege iliyopata ajali siku ya Jumatano. Taasisi hiyo ilisema hapakuwa na manusura katika ajali hiyo.

Urusi yasema imedungua ndege 42 zilizorushwa Moscow kutoka Ukraine 

Moja ya ndege za kivita zisizokuwa na rubani aina ya Punisher ya Ukraine Picha: SERGEI SUPINSKY/AFP

Urusi imesema Ukraine imerusha kombora kuelekea mji mkuu wa Moscow na kuishambulia Crimea kwa takriban ndege 42 zisizokuwa na rubani, ikilitaja tukio hili kuwa moja ya mashambulio mabaya ya angani yaliyoratibiwa na Ukraine dhidi yake.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema makombora aina ya S-200 yaliyovurumishwa katika eneo la Kaluga linalopakana na Moscow, yalidunguliwa kupitia mifumo ya ulinzi wa anga. Gavana wa Kaluga Vladislav Shapsha, alisema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Wizara hiyo ya ulinzi ilisema pia kwamba Crimea, ambayo Urusi iliinyakuwa kutoka kwa jirani yake Ukraine mwaka 2014 ilishambuliwa. Ndege 9 zisizokuwa na rubani zilidunguliwa kupitia mifumo ya ulinzi wa anga na nyngine 33 zilidunguliwa kabla ya kufikia malengo yake baada ya kuzuiwa na mitambo ya kielektroniki. 

Biden na Zelensky wajadili mafunzo ya ndege za F-16

Hata hivyo Ukraine bado haijatoa tamko lolote juu ya hili na kwa kawaida huwa haitoi tamko au kukiri kuhusika na mashambulizi ndani ya Urusi au katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi ndani ya Ukraine.

Ukraine imesema kuharibu miundo mbinu ya kijeshi ya Urusi itaisaidia katika hatua yake ya kujibu mashambulizi dhidi yake kutoka Kiev yaliyoanza mwezi Juni. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy aliuambia mkutano wa kimataifa wiki hii kwamba vikosi vyake vitaukomboa mji wa Crimea.

Urusi yasema iterejea katika makubaliano ya kusafirisha nafaka

Kwengineko Waziri wa amabo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema nchi yake itarejea katika makubaliano ya kusafirisha nafaka katika bahari nyeusi iwapo nchi za Magharibi zitatimiza wajibu wake kwa Moscow.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei LavrovPicha: Sergei Bobylev/dpa/picture alliance

Putin asema Urusi iko tayari kurejea katika usafirishaji wa nafakai

Akijibu suali lililoulizwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres hapo jana, kuhusu nia ya kurejea katika makubaliano hayo alisema hilo litatimia tu iwapo wajibu katika upande wa Urusi utatekelezwa.

Reuters/dpa/ap

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW