PUTIN AWASILI PARIS
18 Machi 2005Matangazo
TAARIFA YA HABARI 16.00 18-03-05
PARIS:
Rais Vladmir Putin wa Russia,amewasili Paris hii leo na kufanya mazungumzo na rais Jacques Chiraq kabla ya mkutano wao na Kanzela Schröder wa Ujerumani na waziri mkuu wa Spian.
Mkutano wa viongozi hao 4 unalenga kumuimarisha rais Putin na kukuza mahusiano baina ya Moscow na Umoja wa Ulaya.
Putin amepangwa pia kukutana na waandishi vitabu wa Russia wanaohudhuria maonesho ya vitabu mjini Paris.
.