1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Huenda pia Ukraine ilihusika na shambulizi

26 Machi 2024

Wakati Urusi na Ukraine zikiendeleza mashambulizi baina yao, Rais Putin akiri kuwa licha ya kundi la wanamgambo la IS kuhusika na shambulizi la ukumbi wa tamasha huenda pia Ukraine ikawa inahusika na shambulio hilo

Urusi | Putin TV
Rais wa Urusi, Vladmir Putin akilielezea tukio la shambulizi la ukumbi wa tamasha hapo liliouwa watu 130Picha: Kremlin.ru/REUTERS

      
Polisi nchini Ukraine imesema Urusi imefanya shambulizi mapema hii leo katika wilaya ya Pecherskyi lililowajeruhi watu 9 na kufanya uharibifu wa makazi ya watu. Mbali na vita hivyo vinavyoendelea, Urusi imewatuma wachunguzi nchini Tajikistan kuzihoji familia za watu wanne ambao wameshtakiwa kwa kufanya shambulio la kutisha kwenye jumba moja la starehe mjini Moscow.

Soma zaidi: Ukraine yasema imeilenga meli ya kivita ya Urusi katika Bahari Nyeusi

Taarifa ya mkuu wa utawala wa kijeshi mjini Kyiv, Serhii Popko imesema kuwa Urusi imerusha makombora mawili ya masafa marefu kuelekea Kyiv kutoka eneo linalokaliwa na Urusi kimabavu la Crimea.

Picha ya muokoaji wa Ukraine akiwa na hofu baada ya shambulizi la Urusi huko Odesa, UkrainePicha: Ukrainian Emergency Service/AP/picture alliance

Baada ya muda mfupi , vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti zaidi ya mara moja kwamba kumetokea milipuko katika mji wa kusini wa Odesa huku makombora ya Urusi yakishambulia pia mikoa mingine kadhaa. 

Familia za washtakiwa wahojiwa Tajikistan

Usiku wa siku ya Alhamisi ya wiki iiyopita , Urusi ilishambulia Kyiv kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha wiki sita kwa kurusha makombora zaidi ya 24.

Siku iliyofuata ya Ijumaa, Urusi ilianzisha tena mashambulizi makubwa dhidi ya kwa kushambulia moja ya mtambo mkubwa  ya nishati wa Ukraine, na kama  namna ya kulipiza kisasi Ukraine ilifanya mashambulizi katika mkoa wa mpaka wa Urusi wa Belgorod na kupelekea Urusi kutangaza kuwahamisha watoto takriban 9,000 waaoishi katika eneo hilo.

Soma zaidi. Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa ndege za droni

Shambulizi la leo, linakuja siku tatu baada ya watub 130 kuuawawa katia shambulizi la ugaidi katika ukumbi wa tamasha nchini Urusi, shambulizi ambalo wapo wanaondai linahusishwa na vita vyake na Ukraine.

Kwa upande mwingine, maafisa wa Urusi wako nchini Tajikistan kufanya mahojiano na familia za watu wanne ambao wanashtakiwa kwa kufanya shambulizi la ugaidi katika ukumbi wa tamasha nchini Urusi.

Wachunguzi wa Urusi wanaendelea na uchunguzi wao kwa kuwahoji washtakiwa wa tukio hilo la ugaidiPicha: picture alliance/AP

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa,  maafisa wa usalama nchini Tajikistan wamezilete familia za washastakiwa hao katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Dushanbe kutoka miji ya Vakhdat na Gissar, na kutoka wilaya ya Rudaki kwa ajili ya uchunguzi.

Putin: Huenda Ukraine ilihusika na shambulio

Wakati uchunguzi huo unaendelea tayari kundi la kigaidi la Islamic state (IS) imekiri kuhusika na tukio hilo huku pia likichapisha video iayoonyesha jinsi walivyotekeleza mauaji katika ukumbi wa tamasha nchini Urusi.

Akilielezea tukio hilo hapo jana Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema, "Ni mbinu za kutisha, kama nilivyosema hapo awali. Na swali linalotokea hapa ni nani anafaidika na hili? Ukatili huu unaweza tu kuwa kiungo katika mfululizo mzima wa majaribio ya wale ambao, tangu 2014, wamekuwa wakipigana nao. nchi yetu kupitia mikono ya utawala wa wanazi mamboleo huko Kyiv. Na Wanazi, inajulikana , hawajawahi kuwa na wasiwasi kuhusu kutumia njia chafu zaidi na zisizo za kibinadamu kufikia malengo yao."

Rais Putin amekiri pia licha ya wanamgambo wa kiislam kuwa nyuma ya shambulio la hilo lakini pia Ukraine huenda pia ikawa inahusika na shambulizi hilo.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW