1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kufanya mazungumzo na Modi wa India, New Delhi

5 Desemba 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo huko New Delhi.

Indien Neu-Delhi 2025 | Treffen Modi und Putin | Ankunft Putin am Flughafen Palam
Picha: DD/ANI Video Grab

Katika mazungumzo hayo, Putin analenga kuongeza biashara na India ambayo ndiyo mnunuaji wake mkubwa wa silaha na mafuta, wakati ambapo vikwazo vya nchi za Magharibi vinazidi kuyakandamiza mahusiano yao ya miongo kadhaa.

Moscow imekuwa muuzaji mkuu wa silaha kwa India kwa miongo kadhaa na imesema kuwa inataka kununua bidhaa nyingi zaidi za India ili biashara kati yao ifikie dola bilioni 100 ifikiapo mwaka 2030.

Putin yuko katika ziara yake ya kwanza nchini India kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne, wakati ambapo India inafanya mazungumzo na Marekani kwa ajili ya mkataba wa kibiashara, utakaoondoa ushuru mkubwa uliowekwa na Rais Donald Trump katika bidhaa zake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW