1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kufanya ziara ya nadra ya siku mbili Korea Kaskazini

17 Juni 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin atawasili Korea Kaskazini kesho Jumanne kwa ziara ya siku mbili ambayo ni ya kwanza ndani ya miaka 24.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Valentina Pevtsova/Pool Sputnik Kremlin via AP/dpa/picture alliance

Putin anatarajiwa kukutana na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un kwa mazungumzo yatakayojikita katika kutanua ushirikiano wao wa kijeshi huku wakiungana zaidi hasa kufuatia mivutano ya mataifa hayo mawili na Marekani. 

Shirika la habari la Korea limesema Putin atakuwepo nchini humo Jumanne na Jumatano  baada ya kupata mualiko rasmi kutoka kwa Kim Joun Un. 

Soma pia:Kim ausifu uhusiano unaotanuka wa Korea Kaskazini na Urusi

Ziara hiyo inakuja wakati kukiwa na wasiwasi wa kimataifa kuhusu silaha zinazotolewa na Pyongyang kwa Moscow, kuisaidia katika vita vyake na Ukraine ili kupata usaidizi wa kiuchumi na teknolojia itakayoimarisha kitisho cha kim cha silaha za nyuklia na mipango ya makombora. 

Ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili umeongezeka hasa baada ya kim kufanya ziara Urusi na kukutana na Putin mwa mara ya kwanza tangu walipokutana mwaka 2019. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW