1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kuruhusu wakaguzi kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia

20 Agosti 2022

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wametoa wito wa kufanyika ukaguzi huru katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kinachodhibitwa na serikali ya Moscow.

Ukraine I Zaporizhzhia I Saporischschja
Picha: , AKW; Atomkraftwerk, Dmytro Smolyenko/Ukrinform/IMAGO

Taarifa hiyo inatolewa katika kipindi ambacho mapigano yanaripotiwa kuendelea katika maeneo ya karibu na kinu hicho.

Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imessema Rais Putin ameonesha zingatio katika takwa la kuzuru kwa  mwakilishi wa Shiriki la Kimataifa la Nguvu za Atomiki kusafiri kupitia Urusi hadi eneo la nyuklia kina cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

Na kwa mujibu wa Ikulu ya Kremlin, viongozi wote wawili walitoa wito kwa wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu ya Atomiki (IAEA) kukagua mtambo huo "haraka iwezekanavyo na kutathmini hali halisi ya katika eneo hilo".

Wasiwasi wa Putin wa kuvuja mionzo ya nyuklia.

Rais Wladimir Putin wa UrusiPicha: Sergei Savostyanov/TASS/dpa/picture alliance

Putin amenukuliwa akitoa msisitizo kwamba "ushambuliaji kwa makombora unaofanywa na jeshi la Ukraine katika eneo la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia unasababisha hatari ya janga kubwa ambalo linaweza kusababisha kuvuja kwa mionzi ya nyuklia ambayo inaweza kuathiri eneo kubwa".

Mkuu wa shirika hilo IAEA, Rafael Grossi ameipokea vyema taarifa hiyo ya kuungwa mkono kwa mataifa hayo kwa ajili ya kwenda kukagua eeno hilo.

Soma zaidi:Zelensky: UN inapaswa kuhakikisha usalama wa kinu cha nyuklia Zaporizhzhia

Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kilitekwa na wanajeshi wa Urusi mwezi Machi na mapigano ya karibuni yameibua wasiwasi wa kutoka ajali ya kinyuklia kwa ulinganifu wa ile ya Chernobyl.

Vyanzo: AP/AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi