1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKazakhstan

Putin na Xi watazamia kuongeza ushawishi wao mkutano wa SCO

3 Julai 2024

Viongozi wa Urusi na China wako Kazakhstan leo kuhudhuria mkutano wa kilele wa kikanda wenye lengo la kuiongezea nguvu miungano inayoipinga Magharibi na kuimarisha ushawishi wao katika kanda ya kimkakati ya Asia ya Kati.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, kulia, na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev wakizungumza pembenezoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai
Rais wa Urusi Vladimir Putin, kulia, na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev wakizungumza pembenezoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya ShanghaiPicha: Gavriil Grigorov/Sputnik/Kremlin Pool Photo/AP/picture alliance

Rais wa urusi Vladimir Putin amewasili katika Mji Mkuu wa Kazakhstan, Astana, asubuhi ya leo kwa mkutano wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO, ambalo ni kundi linaloongozwa na China na kuyajumuisha mataifa ya Asia ya Kati, India na Iran.

Soma pia: Japan, Korea Kusini zatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Kiongozi wa China Xi Jinping aliwasili huko Kazakhstan hapo jana na viongozi hao wawili wanalitazama shirika hilo la SCO kama chombo muhimu cha kuendeleza malengo yao ya kimkakati katika kanda ya Ulaya na Asia.

Urusi na China wamezidisha uhusiano wao wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake Ukraine.