1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Putin, Pezeshkian waahidi kuimarisha uhusiano

12 Oktoba 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Iran, Masoud Pezekshian, nchini Turkemistan, ukiwa mkutano wa kwanza baina yao.

Turkmenistan Iran Pezeshkian Putin
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran (kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, nchini Turkemistan.Picha: Alexander Shcherbak/SNA/IMAGO

Kwenye mkutano huo wa jana, viongozi hao walisifia kuimarika kwa mahusiano ya kiuchumi ya mataifa yao na mitazamo yao inayofanana kwenye siasa za kilimwengu.

Putin, ambaye nchi yake itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa mataifa ya BRICS mjini Kazan mnamo Oktoba 22 hadi 24 mwaka huu, alimualika Pezeshkian kufanya ziara rasmi, mualiko ambao ulikubaliwa na kiongozi huyo wa Iran.

Soma zaidi: Urusi yafanya mashambulizi 114 Ukraine ndani ya masaa 24

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, IRNA, Pezeshkian alisema kila uchao, mahusiano ya kiuchumi, kitamaduni na mawasiliano yanazidi kuimarika kati ya Moscow na Tehran.

Kuimarika kwa uhusiano huo kunaangaliwa kwa mashaka na mataifa ya Magharibi, ambayo yanayachukulia mataifa hayo mawili kuwa mahasimu wao.