1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Silaha za msaada za Ukraine zinauzwa kwa Taliban

Hawa Bihoga
3 Novemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema baadhi ya silaha za mataifa ya Magharibi zilitolewa Ukraine kama msaada wa kivita zimepatikana njiani zikipelekwa Mashariki ya kati kupitia soko haramu la silaha kwa Taliban.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Gavriil Grigorov/Kremlin Pool/Planet Pix/picture alliance

Putin amesema silaha kwa sasa zinaingia mashariki ya kati zikitokea Ukraine akisisitiza kwamba bila shaka silaha hizo zinauzwa kwa Taliban na kisha kuelekea katika maeneo mengine.

"Bila shaka linafanyika hili. Kwa sababu wanaziuza," Alisema Putin alipokuwa maeketi na maafisa wa ngazi za juu wa serikali yake na wataalamu wa masuala mbalimbali.

Aliongeza kuwa silaha hizo zinauzwa katika maeneo ya Mashariki ya Katina kulitaja kundi la Taliban ni miongoni mwa wanunuaji kabla ya kupelekwa kwingineko duniani.

"Wanaziuza kwa Taliban na kutokea hapo zinakwenda popote. Kila kitu kinanunuliwa na kuuzwa." Alisisitiza Putin.

Tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake nchini Ukraine mnamo Februari 24 mwaka jana, mataifa ya Magharibi yameitumia Ukraine silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Soma pia:Urusi yajiondoa kutoka kwenye uidhinishaji wa kupinga majaribio ya silaha za nyuklia

Ukraine imesema inadhibiti vikali silaha zilizotolewa kwake kwa ajili ya kupambana na vikosi vya Urusi, lakini baadhi ya maafisa wa usalama wa nchi za Maghari wamekuwa wakiibua wasiwasi, na Marekani imekuwa ikiitaka Ukraine kushughulikia suala zima la rushwa.

Mnamo mwezi June mwaka uliopita Mkuu wa shirika la kimataifa la polisi Interpol, Jürgen Stock alionya kwamba baadhi ya silaha za kisasa zilizotolewa kwa Ukraine, zingeliishia mikononi mwa vikundi vya uhalifu.

Hata hivyo ripoti kuhusu vita vya Ukraine na biashara haramu ya silaha iliotolewa na shirika la kimataifa la kupambana na uhalifu wa kupangwa la Global Initiative Against Transnational Organized Crime, ilisema "kwa sasa hakuna utoaji mkubwa wa silaha kutoka katika eneo la vita nchini Ukraine."

Ukraine yaendelea kusaka uungwaji mkono

Waziri wa Mambo ya nje ya Ukraine  Dmytro Kuleba amehudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Berlin, akisaka uungwaji mkono zaidi wa umoja huo kwa ajili ya vita vyake na Urusi, katika wakati ambapo Jumuia ya kimataifa ikijielekeza zaidi katika vita huko Gaza.

Waziri wa Mambo ya nje Ukraine Dmytro KulebaPicha: Ameer Al-Mohammedawi/dpa/picture alliance

Kwa upekee aliishukuru Ujerumani kwa mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ambayo itailinda miji ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya Urusi.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliamua mapema mwezi Oktoba kutosambaza makombora ya Taurus, kwa wakati huu kutokana na hatari ya Ujerumani kuingizwa moja kwa moja kwenye vita.

Soma pia:Waziri Mkuu wa Italia, Meloni, ajikuta mtegoni kwenye simu

Ukraine maafisa wamesema Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizokuwa na rubani kwenye miji ya kimkakati na miundombinu muhimu, na kuonya kuwa huenda Moscow ikaongeza mashambulizi yake kabla ya majira ya baridi kuanza.

Rais Volodymyr Zelensky aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba, jana usiku ndege aina ya shaheds takribana 40 zilivurumishwa kuelekea Ukraine na zaidi ya nusu yake zilidunguliwa.

Urusi imekuwa ikitumia mamia ya ndege aina ya shahed zilizotengenezwa Iran kushambulia maneo yaliolengwa Ukraine tangu vita ilipoanza.

Wasiwasi unazidi kuongezeka kwamba Urusi itaongeza mashambuliziya makombora na ndege zisizo na rubani katika jitihada za kuharibu miundombinu ya nishati ya Ukraine, wakati wa majira ya baridi.

Hata hivyo katika chapicho lake kwenye mitandao ya kijemii Zelensky aliongeza kwamba " watamjibu adui, kwa nguvu."

Viongozi wa Afrika wataka kumaliza mzozo wa Ukraine

02:31

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW