1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Urusi haikatai kufanya mazungumzo na Ukraine.

30 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Moscow haipingi kufanya mazungumzo na Ukraine. Putin amesema mkakati wa amani wa Afrika unaweza kutumika kama msingi wa amani, pamoja na ule uliowasilishwa awali na China.

Russlands Präsident Wladimir Putin gibt eine Pressekonferenz in St. Petersburg
Picha: Sergei Bobylev/TASS/imago imagesTASS

Hata hivyo, amesema ni vigumu kufanyika kwa mazungumzo hayo, wakati Kyiv ikiendeleza mashambulizi.

Soma zaidi: Putin aipongeza Afrika inavyoshughulikia masuala ya kimataifa

Aidha taarifa nyingine zinasema Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya kusaka suluhu ya amani yatakayofanyika mwishoni mwa wiki ijayo huko Jeddah.

Vyombo kadhaa vya habari vimesema wajumbe kutoka Ukraine, mataifa ya magharibi na mengine yanayoendelea watahudhuria, lakini Urusi haitashiriki.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW