Putin: Urusi bado ni mshirika mkubwa wa kibiashara duniani
8 Juni 2024Putin ameyasema hayo siku ya Ijumaa katika mkutano wa 27 wa kimataifa wa kiuchumi wa St Petersburg.
Amesema licha ya vikwazo vyote na ambavyo amevitaja kuwa "visivyo halali" vilivyowekwa na nchi za Magharibi, Urusi inaendeleza ushirikiano wake wa kimataifa na kuifanya kuwa miongoni mwa mataifa yanayoongoza kiuchumi.
Soma pia: Kwanini Umoja wa Ulaya bado unaagiza gesi kutoka Urusi?
Putin ameongeza kuwa karibu robo tatu ya biashara za nje sasa inafanywa na nchi ambazo ni rafiki kwa Urusi. Tangu nchi za Magharibi zilipoweka marufuku ya biashara katika maeneo mengi, Urusi ilijielekeza kiuchumi katika mataifa ya China, India, Afrika na Amerika Kusini.
Nchi za Magharibi zimeiwekea Urusi vikwazo kama hatua ya kuaidhibu kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine.