1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Urusi inaweza kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine

29 Januari 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amesema nchi yake inaweza kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine, lakini amefutilia mbali uwezekano wa kuzungumza moja kwa moja na Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin akizungumza wakati wa kikao cha kila mwaka cha maswali na majibu huko Gostiny Dvor mnamo Desemba 19,2024
Rais wa Urusi, Vladimir PutinPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Putin amesema Urusi iko tayari kwa mazungumzo na wawakilishi wa Ukraine lakini haioni nia yoyote kwa upande wa Ukraine ya kutatua maswala ya kisheria. Rais huyo amesema ikiwa kuna nia ya kujadiliana na kutafuta suluhu ya maafikiano, basi mtu yeyote anaweza kufanya mazungumzo hayo.

Putin asema mazungumzo yanapaswa kuheshimu hali halisi

Awali akizungumzia kuhusu uwezekano wa mazungumzo, Putin, alisisitiza kwamba makubaliano yoyote ya amani yanapaswa kuheshimu hali halisi iliyoko.

Putin: Mazungumzo na Ukraine yanawezekana bila Zelensky

Kiongozi huyo wa Urusi pia alidai kuwa mapigano hayo yanaweza kumalizika ndani ya miezi miwili ama mapema zaidi ikiwa mataifa ya magharibi yatakatiza msaada wao kwa Ukraine.

Zelensky ajibu kauli za Putin

Rais Zelensky, alijibu kauli hizo za Putin kwa kusema kiongozi huyo wa Urusi anaogopa mazungumzo na kuongeza kuwa anatumia mbinu alizoziita kuwa za kijanja kurefusha mzozo huo wa karibu miaka mitatu.

Zelensky amesema kuna fursa ya kuafikia amani ya kweli lakini Putin anatatiza juhudi za kusitisha mapigano.

Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: John Thys/AFP

Ukraine pia imeonya dhidi ya kutengwa katika mazungumzo yoyote ya amani kati ya Urusi na Marekani, na kumshtumu Putin kwa kutaka kutumia vibaya nia njema ya Trump katika mzozo huo.

Jeshi la Ukraine lashambulia kiwanda cha mafuta cha Urusi

Jeshi la Ukraine limesema kuwa shambulizi lake la droni katika kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Urusi limesababisha moto mkubwa na kuongeza kuwa linafanya tathmini ya ukubwa wa uharibifu uliofanyika.

Ukraine yaishambulia Urusi kwa droni 121

Wakati huo huo, shambulizi la droni za Ukraine katika eneo la mpaka la Urusi la Belgorod limesababisha kifo cha mama na mtoto wake wa umri wa miaka miwili. Haya yamesemwa leo na gavana katika eneo hilo Vyacheslav Gladkov.

Urusi yadungua droni za Ukraine

Katika hatua nyingine, Urusi imesema leo kuwa imedungua zaidi ya droni 100 za Ukraine katika shambulizi la usiku kucha huku jeshi la Ukraine likisema kuwa Urusi pia imeishambulia kwa droni usiku kucha.

Raia watatu wauawa huko Kherson kufuatia mashambulizi ya Ukraine

Siku ya Jumanne, jeshi la Urusi lilisema vikosi vyake vimeuteka mji mmoja mkubwa katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kharkiv nchini Ukraine, huu ukiwa ufanisi wa hivi karibu zaidi wa udhibiti wa kimaeneo kwa vikosi vya Urusi vinavyozidi kusonga mbele katika uwanja wa vita .

Urusi yadai kuingia katikati mwa mji wa kimkakati mashariki mwa Ukraine

Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimekikomboa kijiji cha Dvorichna, ambacho kilikuwa na wakazi zaidi ya 3,000 kabla ya mapigano.

Mji huo ulitekwa na Urusimwanzoni mwa vita hivyo mnamo mwaka 2020 kabla ya kutwaliwa tena na Ukraine miezi michache baadaye katika mashambulizi ya kisasi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW