PUTIN - UVUMI ULIOZUKA USITE:
10 Desemba 2003Matangazo
MOSCOW: Rais Vladimir Putin wa Russia,amekanusha uvumi uliozaga kwamba kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake cha "United Russia" katika uchaguzi wa bunge wa hivi karibuni,anataka kuibadilisha katiba ili aweze kuwa madarakani kwa kipindi cha tatu.Kwa mujibu wa shirika la habari "Interfax" mjini Moscow,rais Putin amesema uvumi huo lazima ukome na akaongezea kwamba katiba ya hivi sasa ni msingi wa utulivu wa jamii ya Russia.Katika uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya jumapili yasemekana kuwa vyama vinavyomuunga mkono Putin huenda vikajinykulia theluthi mbili ya kura.Matokeo ya mwisho ya uchaguzi bado hayajulikani.
