1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin yuko ziarani Kazakhstan kuimarisha uhusiano

27 Novemba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko Kazakhstan kwa ziara ya siku mbili inayolenga kuimarisha uhusiano na mshirika wake wa Asia ya Kati.

Hayo ni wakati mivutano ikiongezeka kuhusiana na vita vya Ukraine. Akizungumza kabla ya kutua leo katika mji mkuu wa Kazakhstan Astana, Putin alisifu maadili ya kaitamaduni, kiroho kati ya nchi hizo mbili na akasema yuko tayari kukuza zaidi uhusiano wa kirafiki na kiushirika na Astana. Kazakhstan ni mwanachama wa muungano wa usalama unaoongozwa na Moscow wa CSTO lakini imeelezea wasiwasi kuhusu mzozo wa takriban miaka mitatu wa Urusi na Ukraine ambao Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev amekataa kuuunga mkono. Mivutano imeongezeka kati ya Moscow na nchi za Magharibi kuhusiana na vita vya Ukraine, huku Urusi ikirusha kombora la majiribio la kasi kubwa dhidi ya jirani yake wiki iliyopita. Nayo Kyiv ilijibu kwa mara ya kwanza kwa kurusha kuelekea Urusi makombora ya masafa marefu yaliyotengenezwa na Marekani na Uingereza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW