1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin ziarani Ghuba

6 Desemba 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi anafanya ziara fupi katika eneo la Ghuba ambapo anazuru Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu katika eneo hilo la Ghuba.

Rais Vladimir Putin wa Urusi (kushoto) akipokea na Waziri wa Mambo ya Nje ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdullah bin Zayed Al Nahyan.
Rais Vladimir Putin wa Urusi (kushoto) akipokea na Waziri wa Mambo ya Nje ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdullah bin Zayed Al Nahyan.Picha: Andrei Gordeyev/Sputnik/Kremlin via AP/picture-alliance

Ziara hiyo ya Putin inalenga kutafuta uungaji mkono katika Mashariki ya Kati kutoka kwa madola hayo mawili yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani na ambayo ni washirika wa Marekani, wakati vita vyake na Ukraine vikiendelea.

Putin aliwasili Abu Dhabi na kulakiwa na kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohammed bin Zayed. 

Soma zaidi: Waziri wa nje wa Marekani Hillary Clinton ziarani katika Ghuba

Wakati wa mkutano na kiongozi huyo wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Putin alisema kuwa uhusiano kati ya Urusi na Umoja huo uko katika kiwango cha juu ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Soma zaidi: Merkel ziarani Saudi Arabia

Putin alisifu uhusiano baina ya nchi hizo mbili na kuutaja kuwa wa kipekee kihistoria na wakati huo huo kumualika Zayed kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi la BRICS mwakani huko Kazan. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW