1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin:Hakuna matokeo ya kukasirisha kutoka kwa adui

Hawa Bihoga
21 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba mashambulizi ya vikosi vya Kyiv yaliofanywa ili kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi huko kusini, na mashariki mwa Ukraine, yalishindwa licha ya msaada wa mataifa ya Magharibi.

Russland Präsident Putin in Moskau
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Russian President Press Office/dpa/picture alliance

Katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Kremlin Putin amesema "kwa namna yoyote,bado hakuna matokeo ya kukasirisha" kutokana na mashambulizi ya adui.

Ameongeza kwamba, mataifa ya Magharibi ambayo yamekuwa yakiunga mkono serikali ya Kyiv, yamekatishwa tamaana matokeo na kile alichokitaja matamshi ya viongozi wa Ukraine mwezi uliopita.

Rais Putin amesema jeshi la Ukraine limepata hasara kubwa wakati wa jaribio lake la kushambulia, huku nchi za Magharibi zikiendelea kudumisha usambazaji wa silaha kwa wingi, ikiwa ni pamoja na makombora.

Soma Pia:Baerbock: Putin anapaswa kuwajibishwa kwa uhalifu wa kivita

Aliongeza Putin kwamba vikosi vya jeshi la Ukraine vimepata hasara kubwa katika mashambulizi ya kujitoa mhanga kiasi cha makumi kwa maelfu ya wanajeshi.

"Hali inazidi kuwa ngumu kwa serikali kutuma nyongeza ya vikosi kwenye uwanja wa mapambano." Alisema Putin katika hotuba yake ya video.

Moscow yazidisha mashambulizi Ukraine

Vikosi vya Moscow bado vinashikilia maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine na baadhi ya maeneo yakimkakati, huku vikosi vya Ukraine vikiendelea kujibu mashambulizi ya Urusi.

Mapema wiki hii mmoja wa afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Kyiv alisema kwamba operesheni hiyo itakuwa "ya muda mrefu na ngumu" na kutoa wito kwa washirika kutuma magari zaidi ya kivita na silaha.

Urusi inaonesha hali ipo sawa baada ya uasi wa wagner

01:52

This browser does not support the video element.

Soma pia:Putin: Urusi ina hifadhi ya kutosha ya mabomu ya mtawanyiko kujibu mashambulizi

Putin pia ameishutumu Poland ambayo ni mshirika wa karibu wa Ukraine, na kuwashutumu viongozi wake kwa kujaribu "kuingilia moja kwa moja mzozo" huo.

Serikali ya Poland ambayo ni mwanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya, ilitangaza kupeleka wanajeshi wake huko Mashariki, kutokana na uwepo wa kikosi cha mamluki cha Urusi Wagner katika nchi jirani ya Belarus.

Urusi:Tunafanyia kazi makubaliano ya usafirishaji nafaka

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Vershinin amesema Urusi inafanyia kazi njia mpya za usafirishaji wa nafaka,baada ya Moscow kutorefusha makubaliano katika mpango wa mauzo ya nafaka katika Bahari Nyeusi mapema wiki hii.

Makubaliano hayo, yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki, yalilenga kusaidia kuzuia mzozo wa chakula duniani kwa kuruhusu nafaka zilizozuiwa na vita nchini Ukraine kusafirishwa kwa usalama kutoka bandari za Bahari Nyeusi.

Soma pia:Urusi yashambulia bandari za Ukraine baada ya kujiondoa katika mkataba wa usafirishaji salama wa nafaka katika Bahari Nyeusi

Naibu waziri Vershinin amesisitiza kwamba lazima kuwe na hakikisho kwamba meli hazibebi kitu cha tofauti akimaanisha umuhimu wa ukaguzi, ili kuwe na uhalali wa makubaliano hasa baada ya kuwepo kwa mashambulizi kadhaa aliyoyataja ya kigaidi.

Ameongeza kuwa hakutakuwa na njia salama za kiutu katika bahari, na badala yake kwa sasa kinachoongezaka ni maeneo hatari ya kijeshi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW