PYONGYANG: Kinu cha nyuklia kufungwa
25 Juni 2007Matangazo
Mkuu wa kundi la wakaguzi wa umoja wa mataifa wa nyuklia ameawasili mjini Beijing akiwa safarini kuelekea mjini Pyongyang, Korea Kaskazini anakotarajiwa kushuhudia kufungwa kwa kinu cha nyuklia.
Olli Heinonen naibu mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu za nyuklia amesema kwamba kituo cha Yongbyon kitafungwa kabisa.
Ziara ya hapo kesho itakuwa ya kwanza kufanywa na wachunguzi wa umoja wa mataifa nchini Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka mitano.
Shughuli ya kukifunga kinu hicho cha nyuklia inaambatana na makubaliano ya pande sita ya mwezi Februari.