PYONGYANG Korea Kazkazini kusiriki tena katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa silaha za kinuklia.
23 Februari 2005Matangazo
Katika hatua ya kushangaza, kiongozi wa Korea Kazkazini, Kim Jong wa pili amesema taifa lake liko tayari kushiriki tena katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa silaha za kinuklia, iwapo masharti fulani yatazingatiwa. Kim amenukuliwa na shirika la habari la Pyongyang akimwambia mwanadiplomasia wa China ambaye yumo ziarani nchini humo, kwamba mazungumzo hayo huenda yaanze tena wakati wowote ikiwa Marekani itaonyesha uaminifu unaoweza kutegemewa. Mapema mwezi huu, Korea Kazkazini ilitangaza wazi kwa mara ya kwanza kuwa ina miliki silaha za kinuklia, lakini ikataa wakati huo kushiriki katika mazungumzo na Marekani, Korea Kusini, China, Japan na Russia.