PYONGYANG-Korea ya kaskazini yathibitisha kuzuka kwa homa ya ndege.
27 Machi 2005Serikali ya Korea ya Kaskazini imethibitisha kutokea mripuko wa homa kali ya mafua ya ndege katika maeneo yake yanayojishughulisha na ufugaji wa kuku.Ofisa wa Shrika la habari la Korea ya Kaskazini,ameripotiwa kuwanukuu watu wa mamlaka zinazohusika na karantini,wakitoa ripoti ya kuzuka kwa maradhi hayo,katika mashamba matatu yanayofuga kuku katika mji mkuu Pyongyang.Ripoti hiyo imeeleza maelfu ya kuku wameangamizwa ili kudhibiti ueneaji wa maradhi hayo.
Ripoti hiyo imeendelea kueleza kuwa hakuna mfanyakazi yeyote katika mashamba hayo aliyeambukizwa maradhi ya homa ya ndege.
Korea ya Kaskazini ulipozuka ugonjwa huo mwaka 2003,ilijitangaza kutokumbwa na kadhia hiyo,ambapo maradhi hayo yalisambaa zaidi katika maeneo ya Mashariki mwa Bara la Asia na kuuwa 48 na mamilioni ya kuku,ndege,bata na jamii ya hiyo kwa mamilioni.