PYONGYANG: Makombora ya masafa mafupi yajaribiwa
8 Juni 2007Matangazo
Korea ya Kaskazini imejaribu makombora mawili ya masafa mafupi nje ya pwani yake ya magharibi. Maafisa wa Kimarekani wamesema,jeribio hilo halitosaidia hali ya hivi sasa,wakati ambapo Pyongyang inatazamiwa kuonyesha ushahidi kuwa inasitisha mradi wake wa nyuklia.Mwishoni mwa mwezi Mei,Korea ya Kaskazini ilifanya jeribio kama hilo nje ya mwambao wake wa mashariki.Korea ya Kusini na Marekani zilipuza jeribio hilo kama ni zoezi la kijeshi la kawaida.