Pyongyang. Rais wa Korea ya kusini akataa mwaliko ya kubaki zaidi Korea ya kaskazini.
4 Oktoba 2007Matangazo
Rais wa Korea ya kusini Roh Moon-hyun amekataa mualiko kutoka kwa kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il kurefusha ziara yake ya hivi sasa nchini humo kwa siku moja. Wakati huo huo , hata hivyo , Roh ameeleza kuridhishwa na hatua za maendeleo katika mazungumzo, ambayo yalikuwa na nia ya kupunguza hali ya wasi wasi baina ya Korea hizo mbili. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja mwishoni mwa mkutano wao wa siku tatu utakapomalizika siku ya Alhamis. Huu ni mkutano wa pili baina ya viongozi hao wa Korea tangu mwishoni mwa vita vya Korea katika mwaka 1953.