Pyongyang. Wachunguzi wa kinuklia kurejea Korea ya kusini.
14 Machi 2007Matangazo
Kiongozi wa shirika la umoja wa mataifa la kinuklia Mohammed El Baradei amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Korea ya kaskazini mjini Pyongyang.
Kiongozi huyo wa shirika la kimataifa la nishati ya kinuklia anamatumaini ya kupata ruhusa ya Korea ya kaskazini ili kutuma wachunguzi wa kinuklia kurejea tena nchini humo baada ya kupigwa marufuku mwaka 2002.
ElBaradei ameanza ziara yake hiyo mwezi mmoja baada ya makubaliano ya kihistoria yaliyoleta matumaini kuwa Korea ya kaskazini hatimaye itaachana na mpango wake wa kinuklia.
Chini ya makubaliano hayo Korea ya kaskazini imesema itawaruhusu wachunguzi kurejea nchini humo na kufunga vituo vya kinuklia katika muda wa siku 60 lakini baada ya kupata msaada wa mafuta.