PYONGYANG: Wajumbe wa Umoja wa Matafia wawasili Korea Kaskazini
26 Juni 2007Matangazo
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamewasili mjini Pyongyang Korea Kaskazini katika ziara yao ya kwanza tangu walipoamriwa waondoke nchini humo yapata miaka mitano iliyopita.
Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa ukiongozwa na Olli Heinone, naibu mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kuzuia utapakazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, unatarajiwa kusimamia kufungwa kwa kinu cha nyuklia cha Yongbyon.
Tume hiyo imeenda mjini Pyongyang kama sehemu ya makubaliano ya mwezi Februari mwaka huu yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mataifa sita mjini Beijing China, ambapo Korea Kaskazini iliahidi kukifunga kinu chake cha Yongbyon ikiwa itasaidiwa na nishati na kuwa na uhusiano wa kidiplomasia.