PYONGYANG: Wakaguzi wa IAEA wamewasili Korea ya Kaskazini
28 Julai 2007Matangazo
Tume ya pili ya wakaguzi wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa,IAEA imewasili Korea ya Kaskazini.Wakaguzi hao watasimamia hatua ya kufunga mtambo wa nyuklia wa Yongbyon.Serikali ya Pyongyang imekubali kusitisha mradi wake wa nyuklia uliozusha mabishano na badala yake, inapewa misaada ya kiuchumi na kiutu.