1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Pyongyang yafanya mazoezi ya mbinu za shambulizi la nyuklia

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Korea Kaskazini imefanya mazoezi ya kimbinu ya shambulio la nyuklia jana Jumamosi ambayo yalijumuisha makombora mawili ya masafa marefu.

Korea Kaskazini | Kim Jong-Un
Moja ya kombora la Korea Kaskazini wakati wa mazoezi yakePicha: YNA/picture alliance

Korea Kaskazini imefanya mazoezi ya kimbinu ya shambulio la nyuklia jana Jumamosi ambayo yalijumuisha makombora mawili ya masafa marefu. 

Shirika la habari la nchi hiyo KCNA, limeripoti kwamba mazoezi hayo yalifanyika mapema jana kama ishara ya kutoa onyo kwa maadui kwamba nchi hiyo itakuwa tayari endapo kutatokea vita vya nyuklia.

Aidha, Pyongyang imeapa kwa mara nyingine kwamba itaimarisha uwezo wake wa kijeshi ili kukabiliana na Marekani na Korea Kusini. Jaribio hilo la Korea Kaskazini linafanyika mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka baina ya Marekani na Korea Kusini.

Vyombo vya habari pia vimeripoti kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alifanya ukaguzi wa viwanda vya ujenzi wa meli na utengenezaji wa silaha.