1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Pyongyang yasema Marekani imethibitisha uadui usiobadilika

22 Novemba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia wa kipindi cha nyuma kati ya Pyongyang na Marekani ulithibitisha uadui usiobadilika dhidi ya nchi yake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un akitoa hotuba wakati wa mkutano mjini Pyongyang mnamo Novemba 15, 2024
Kiongozi wa Korea Kaskazini- Kim Jong UnPicha: Korean Central News Agency/Korea News Service via AP/picture alliance

Kim ameyasema hayo Alhamisi wakati wa maonesho ya ulinzi yalioonesha baadhi ya mifumo ya silaha yenye nguvu zaidi ya Korea Kaskazini.

Kauli yake inakuja ikiwa ni miezi michache kabla ya Donald Trump kuingia rasmi madarakani kama rais wa Marekani. 

Katika muhula wake wa kwanza wa uongozi, Trump aliwahi kukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini mara tatu lakini Marekaniilishindwa kupiga hatua kubwa katika kuishawishi nchi hiyo ipunguze silaha zake za nyuklia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW