PYONGYANG:Mzozo wa Mpango wa Nuklia wa Korea Kaskazini
3 Agosti 2005Matangazo
Mazungumzo ya nchi sita juu ya mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini yaliyoingia siku yake ya nane hapo jana yameshindwa kufaulu.
Korea Kaskazini imesema mazungumzo hayo bado hayajapiga hatua yakuelekea mafanikio.
Japan upande wake inasema Korea Kaskazini bado haijakubali kwamba ina mpango wa kurutubisha madini ya Uranium licha ya kudai kuwa na silaha za Kinuklia.
Korea kaskazini inasema hadi pale Marekani na mataifa mengine yatakapo ihakikishia msaada na usalama wa kijeshi ndipo itakapo komesha shughuli zake za kinuklia.