1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Qatar inatumai kuwa na utulivu zaidi kati ya Israel-Hamas

27 Novemba 2023

Qatar inatumai kurefusha makubaliano ya usitishaji mapigano baina ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas zaidi ya siku nne zilizokubaliwa sasa

Shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 25, 2023
Shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Francisco Seco/AFP/Getty Images

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed Al-Ansari amesema kuwa wanataka kutumia makubaliano ya sasa ili kurefusha usitishwaji mapigano utakaoruhusu mateka wote kuachiliwa.

Kundi la kwanza na la pili la mateka wa Israel liliachiwa juzi na jana huku kundi la tatu likitarajiwa kuachiwa huru leo Jumapili. Makubaliano ya sasa ambayo yameshuhudia pia Israel ikiwaachia wafungwa wa Kipalestina, yanatarajiwa kudumu hadi kesho Jumatatu.

Soma pia: Usitishwaji mapigano kuanza Gaza, mateka kuachiwa

Makubaliano hayo pia yameruhusu malori yapatayo 300 ya chakula, vifaa vya matibabu na mafuta kuingia  Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo tawi la kijeshi la Hamas, limethibitisha vifo vya makamanda wake wanne katika mapiganao ya Gaza kabla ya makubaliano ya sasa. Miongoni mwao ni kamanda wa Brigedi ya Gaza Kaskazini Ahmed al-Ghandour na mjumbe wa Baraza la Kijeshi la Hamas. Jeshi la Israel lilisema siku 10 zilizopita kwamba al-Ghandour na Ayman Siyyam, waliohusika na mashambulizi ya roketi, waliuawa katika shambulio la mabomu kwenye njia za chini ya ardhi huko Gaza.