1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaQatar

Qatar yathibitisha juhudi za kidiplomasia na Iran zaimarika

3 Februari 2026

Wizara ya mambo ya nje ya Qatar imesema juhudi kubwa za kidiplomasia zinaendelea kati ya Iran, Qatar na mataifa mengine ya kikanda baada ya Tehran kuthibitisha mazungumzo na Marekani.

Uingereza London 2026 | Maandamano dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya ubalozi wa Marekani
Watu waliojitokea kuandamana kuupinga utawala wa Iran nje ya ubalozi wa Marekani na kutolea wito Marekani na Uingereza kuwaunga WairanPicha: Martin Pope/SOPA Images/IMAGO

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Majed al-Ansar amewaambia wandishi wa habari kuwa juhudi zinaendelea kwa nguvu kubwa kwa wakati huu na Qatar imekuwa ikishirikiana na majirani zao wakiwemo Misri, Oman, Saudi Arabia na Uturuki.

Amesema "Hii imekuwa inatokea katika katika siku chache zilizopita, siyo na Qatar, lakini pia na pande zote za kikanda. Bila shaka kuna mawasiliano ya ngazi ya juu, kama ambavyo mmeona, yanayolenga kupunguza mzozo katika kanda na kuzuwia kurudi kwenye uchochezi."

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alisema Jumanne kuwa amemuagiza waziri wa mambo ya nje kuanzisha majadiliano ya haki na usawa na Marekani katika ishara ya kwanza kutoka Tehran kwamba inataka kujaribu kufanya majadiliano wakati mzozo ukipamba moto na Washington, kufuatia ukandamizaji mkali kwenye maandamano ya kitaifa mwezi uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW