1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar yazihimiza Marekani na Iran kuzingatia mazungumzo

13 Aprili 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, amemwambia leo mwenzake wa Iran Abbas Araghchi kwamba nchi hiyo na Marekani zinapaswa kushirikiana vyema katika juhudi za upatanishi.

Qatar Doha | Mohammed bin Abdulrahman al-Thani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani Picha: Qatari Foreign Ministry/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Qatar imesema wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu, Al Thani alitoa wito kwa Araghchi na kusisitiza haja ya kufungua njia za baharini, kuhakikisha uhuru wa safari za meli.

Wakati huo huo,  Bahrain imemuita leo balozi wa Iraq nchini humo kuhusu mashambulizi ya droni inayodai yalirushwa kutoka nchini humo kuelekea ufalme huo na mataifa mengine ya Ghuba licha ya usitishaji wa mapigano kati ya Iran na Marekani.

Pia imeitaka nchi hiyo kushughulikia vitisho na mashambulizi hayo haraka iwezekanavyo na kwa uwajibikaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW