1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar yaendeleza juhudi za kuachiliwa mateka wa Israel

15 Novemba 2023

Qatar imezitolea wito pande zinazohusika katika mzozo wa Gaza, Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kuwaachia mateka, ikionya kwamba hali inayoendelea Gaza inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Israel -Maandamano ya jamaa waliotekwa
Mwandamanaji akiwa ameshika picha ya ndugu yake aliyetekwa na HamasPicha: Ahmad Gharabli/AFP/Getty Images

Qatar imezitolea wito pande zinazohusika katika mzozo wa Gaza, Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kuwaachia mateka, ikionya kwamba hali inayoendelea Gaza inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Qatar, Majed bin Mohammed Al-Ansari amesema hali inayozidi kuzorota katika Ukanda wa Gaza inatatiza juhudi za upatanishi.Duru zaarifu juu ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kwa muda Ukanda wa Gaza

Taifa hilo limeongoza juhudi za mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na usitishaji mapigano kwa muda sasa.

Itakumbukwa kwamba siku ya Jumatatu, kundi la Hamas lilidai kuwa, Israel imeomba kuachiliwa huru kwa wanawake na watoto wapatao 100 kwa mabadilishano ya watoto 200 wa Kipalestina na wanawake wanaoshikiliwa katika jela za Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW