Qatar:Operesheni za Israel zazorotesha mazungumzo ya amani
14 Mei 2024Matangazo
Waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani ameuambia mkutano wa kiuchumi unaofanyika nchini humo, kwamba katika kipindi cha wiki chache zilizopita, wameshuhudia hatua zikipigwa lakini kwa bahati mbaya mambo hayakwenda vizuri na hivi sasa wamefikia katika hatua ya kuelekea kwenye mkwamo. Qatar imekuwa ikishirikiana na Misri na Marekani kwa miezi kusimamia mazungumzo ya upatanishi kati ya pande hizo mbili. Israel imeendelea kulishambulia kundi la Hamaskatika mji wa Rafah ,licha ya kauli za kuonywa na Marekani dhidi ya kufanya mashambulizi makubwa katika mji huo wa Kusini mwa Ukanda wa Gaza unaokaliwa na maelfu ya Wapalestina.