1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUITO: Hatimae rais wa Ecuador Lucio Guitierez amwaga unga.

21 Aprili 2005

Rais Lucio Gutierrez wa Ecuador ameng’olewa mamlakani na bunge la congress huku wanajeshi wa nchi hiyo wakichukua hatua ya kusimamisha kumuunga mkono.

Katika muda wa wiki moja Mji wa Quito ulizongwa na maandamano ya kumtaka rais Lucio ajiuzulu kutokana na kuingilia kwake shughuli za mahakama kuu ya nchi hiyo.

Wabunge 60 kati ya jumla ya wabunge 100 wa congress walipiga kura ya kumuachisha rais Lucio wadhfa wa urais kwa kile walichokitaja kuwa ameyatelekeza majukumu yake.

Makamu wa rais wa Ecuador Alfredo Palacio tayari ameshaapishwa kama rais mpya.

Upinzani unamlaumu kiongozi huyo aliyetimuliwa mamlakani kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW