1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Mkutano juu ya uhamiaji umeanza leo nchini Moroko

10 Julai 2006

Mawaziri wa mambo ya kigeni na wa mambo ya ndani kutoka mataifa 57 ya Ulaya na Afrika wameanza mkutano wao wa siku mbili mjini Rabat nchini Moroko kujadili mbinu za kulitanzua tatizo la wahamiaji wasio halali barani Ulaya.

Mawaziri hao wanapania kudumisha hatua za usalama zitakazozuia uhamiaji na wakati huo huo kuboresha hali ya kiuchumi katika mataifa wanakotokea wahamiaji.

Takriban wahamiaji 9,000 wamekamatwa wakijaribu kuingia Ulaya katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu, zaidi ya idadi yote ya mwaka jana wa 2002.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW