1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Waafrika 6 wauawa mpakani Melilla

8 Oktoba 2005

Vyombo vya habari nchini Morocco vimeripoti kuwa Waafrika 6 wameuawa katika mapambano yaliozuka na askari jeshi wa Kimorocco wanaolinda uzio wa mpaka unaozunguka eneo la Hispania la Melilla.Katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni,wahamiaji wa Kiafrika kwa maelfu,mara kwa mara,wamejaribu kujipenyeza Melilla na eneo lingine la Hispania la Ceuta,kwenye pwani ya kaskazini ya Morocco.Wiki iliyopita,wakimbizi 5 walipoteza maisha yao walipojaribu kuvuka mpaka na kuingia Ceuta.Hispania imewarejesha Morocco Waafrika 70,kuambatana na sera yake mpya ya kuwafukuza watu wanaoingia maeneo yake kwa njia isiyo halali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW