1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT. Wafungwa 7,000 waachiliwa huru nchini Moroko.

15 Aprili 2005

Mfalme Mohammed wa Moroko amewaachilia huru wafungwa zaidi ya 7,000 kuadhimisha kutahiriwa kwa mwanawe wa kiume wa miaka 23. Idadi hiyo inawajumulisha wafungwa 523 waliowagonjwa sana, wanawake wajawazito 19, wazee 20, vijana 629 waliopokea mafunzo wakati wa kifungo chao, na wafungwa 5,888 ambao walikaribia kumaliza vifungo vyao. Kati ya wale walioachiliwa ni wafungwa 26 wa kigeni, ijapo uraia wao haukatangazwa. Wengi wa wafungwa nchini Misri wanatokea barani Ulaya. Hii ni mara ya pili kwa mfalme Mohammed kuwaachilia wafungwa wengi, mara ya kwanza ikiwa wakati alipowaachilia wafungwa zaidi ya 8,000 kuadhimisha harusi yake na mhandisi wa komputa, malkia Lalla Salma.