1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT:Mawaziri wajadili mikakati ya kuzuia uhamiaji wa kinyume cha sheria

11 Julai 2006

Mawaziri wa mambo ya ndani na wa mambo ya nchi za nje kutoka nchi takriban 60 za Africa na Ulaya wanakutana katika mji mkuu wa Morocco Rabat, ili kuzungumzia njia za kukabiliana na uhamiaji wa kinyume cha sheria barani Ulaya.

Mawaziri hao wanajadili hatua za kuimarisha usalama ili kuzuia mtiririko wa wahamiaji wanaongia barani Ulaya , sambamba na hatua za kuzifanya hali za maisha na za kiuchumi za nchi ambapo watu hao wanatoka ziwe bora.

Mnamo kipindi cha miezi sita iliyopita watu alfu 9 kutoka barani Africa walikamatwa, walipokuwa njiani wakijaribu kuhamia katika nchi kadhaa za Ulaya kinyume ch sheria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW