1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Radi yaua 14 katika Kanisa kambi ya waikimbizi Uganda

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Polisi nchini Uganda imesema watu 14 wameuawa na radi katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Tukio hilo lilitokea Jumamosi katika wilaya ya Lamwo.

Kijiji cha Yumbe Uganda
Kijiji cha Yumbe UgandaPicha: Sheila Mysorekar/DW Akademie

Msemaji wa polisi Kituuma Rusoke amesema watu wengine 34 walijeruhiwa, na kuongeza kuwa hadi sasa, waathirka hawajafahamika. 

Wakaazi katika kambi ya wakaazii ya Palabek, ambayo hasa ina wakimbizi kutoka Sudan Kusini, walikuwa wakihudhuria ibada ya misa katika kanisa lilijengwa kwa vyuma wakati radi ilipopiga. 

Soma pia:Kazakhstan yapiga kura ya kujenga mtambo wa nyuklia

Matukio ya hatari ya radi huripotiwa mara kwa mara katika taifa hilo wakati wa msimu wa mvua. Rusoke alisema hakuna ripoti ya moto kuzuka kufuatia mkasa huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW